Thursday 8 September 2016

MAKALA KUHUSU PARACHICHI NA USINDIKAJI WAKE.

Maparachichi ni moja ya zao la matunda ambalo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Mbeya,
Kilimanjaro, Morogoro, Kigoma, Kagera, Arusha na Tanga. Wastani wa uzalishaji ni tani 5574.4 kwa mwaka. Zao hili ni muhimu katika lishe kwani lina mafuta na protini kwa wingi kuliko matunda yote yanayoliwa nchini.


MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI
Ili kupata matunda yenye ubora unaotakiwa ni muhimu kuzingatia kanuni za kilimo bora za
uzalishaji wa maparachichi. Hii ni kwa sababu ubora wa mazao baada ya kuvunwa
hutegemea jinsi mazao hayo yalivyozalishwa. Baadhi ya kanuni za kuzingatia ni kama
zifuatazo:
  • Chagua aina bora kupanda kulingana na mahitaji ya soko.
  • Dhibiti magonjwa na wadudu ili kupata mazao mengi na bora yanayoweza kuhifadhiwa kwa
    muda mrefu.
  • Pia dhibiti magugu na safisha barabara ndani ya shamba ili kurahisisha kazi ya kuvuna na kusafirisha mazao.
MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA
  • Maandalizi yanayotakiwa kabla ya kuvuna ni kama yafuatayo:


Kukagua shamba.
  • Kagua shamba ili kuona kama matunda yamekomaa.
  • Kwa kawaida maparachichi hukomaa katika kipindi cha miezi sita hadi tisa kutoka maua yanapochanua.
Dalili za maparachichi yaliyokomaa.
Si rahisi kutambua maparachichi yaliyokomaa kwa kuangalia rangi ya tunda. Hivyo ni muhimu kuzingatia muda wa kukomaa. Maparachichi yakivunwa yangali machanga hunyauka na kuoza. Ni vyema kuchuma parachichi moja au mawili na kuyakata kuona rangi yake kwa ndani ambayo itadhihirisha kukomaa kwa matunda.


KUANDAA VIFAA, VYOMBO VYA KUVUNIA, KUFUNGASHIA NA KUSAFIRISHIA.
  • Ngazi
  • Vikapu
  • Vichumio
  • Makasha ya mbao
  • Mifuko
  • Matenga
  • Matoroli
  • Magari
  • Baiskeli
  • Matela ya matrekta.
KUVUNA.
Njia bora ya kuvuna ni kutumia Mikono.
  • Kwa miparachichi mifupi chuma tunda pamoja na kikonyo chake kwa kutumia mkono.
  • Kwa miparachichi mirefu chuma matunda kwa kutumia kichumio maalum au kwea mti kwa
    kutumia ngazi na chuma kwa mkono.
  • Chuma matunda yaliyokomaa tu. Uvunaji wa matunda ambayo hayajakomaa husababisha matunda kusinyaa na nyama ya ndani kuwa na kambakamba wakati wa kuivisha.
  • Acha kikonyo chenye urefu wa sentimeta moja kwenye tunda
  • Vuna wakati wa asubuhi au jioni ili kuepuka jua kali linaloweza kubabua matunda.
  • Weka kwenye sehemu yenye kivuli. Jua hubabua matunda na huongeza kasi ya kuoza.
  • W akati wa kuvuna hakikisha matunda hayadondoki chini.
Kuchambua, Kusafisha na Kupanga Madaraja.
Shughuli ya kuchambua, kusafisha na kupanga madaraja ifanyike kivulini ili kuepuka jua
ambalo linaweza kubabua matunda.

Kuchambua.
Ni muhimu kuchambua maparachichi ili kutenga yaliyoshambuliwa na wadudu, magonjwa na yaliyopasuka au kuchubuka au yenye makovu.
  • Matunda yaliyooza na yenye wadudu hayafai kwa matumizi hivyo yafukiwe, ili kuepusha ueneaji wa magonjwa.
  • Matunda yaliyopasuka, kuchubuka kidogo au kubonyea yatumike haraka.
  • Matunda mazuri ambayo hayajapata madhara yoyote yawekwe kwa ajili ya kusindikwa, kutumika au kuuzwa.
Kusafisha.
Baada ya kuchambua maparachichi yaoshwe kwa maji safi ili kuondoa uchafu na masalia
ya madawa.

Kupanga madaraja.
  • Kabla ya kupanga madaraja ni muhimu kupunguza vikonyo vya matunda. Punguza na ubakize vikonyo vyenye urefu wa milimita tano. Vikonyo virefu zaidi kufanya ufungashaji kuwa mgumu.
  • Upangaji wa madaraja hufuata uzito na ukubwa wa matunda.
  • Tenganisha matunda yaliyoharibika umbo, yaliyochubuka au yaliyoiva kupita kiasi, au yenye makovu.
  • Inashauriwa kunyunyiza nta kwenye maparachichi ili kupunguza upotevu wa maji, kurefusha muda wa kuhifadhi na kufanya yavutie kwenye soko.
Kufungasha.
Vifungashio vinavyotumika kufungashia maparachichi ni kama vilivyoonyeshwa hapo juu,
baahdi yake ikiwa ni:
  • Makasha ya mbao
  • Matenga--Ufungashaji wa kwenye matenga yaliyosukwa vizuri ili kuruhusu hewa kupita yanatumika katika ubebeaji wa mboga na matunda. Inashauriwa kupanga bidhaa vizuri ndani ya matenga hayo baada ya kutanguliza vitu visafi kama makaratasi au nyasi safi na kavu au majani safi na makavu ya migomba ili kuzuia michubuko ya matunda yanapogongana. Vifaa vya kutanguliza kwenye vifungashio lazima viwe safi, visivyoingiza vimelea vya ugonjwa kwenye matunda.

Kusafirisha.
Baada ya kufungasha matunda, inashauriwa kupanga vizuri ndani ya vyombo vya usafiri na
kutozidisha ujazo kwenye vyombo hivyo ili kuepusha upoteaji unosababishwa na kumwagika au kupasuka kwa matunda na kuchubuka. Barabara nyingi za vijijini sio za lami na ujazo mkubwa wa vifungashio ndani ya magari ya kusafirisha mazao hadi mijini husababisha upotevu mkubwa wa mboga na matunda. Vilevile uangalifu unahitajika wakati wa kupakia na kupakua.

Kuhifadhi.
  • Maparachichi huweza kuhifadhiwa kwenye joto lipatalo nyuzi 10 hadi 18 za Sentigredi ambapo hudumu kwa kipindi cha wiki tatu bila kuharibika.
  • Matunda yakihifadhiwa kwenye nyuzi joto 20 hadi 25 za Sentigredi huiva haraka na huhifadhika katika muda mfupi (siku 5 hadi 15).
KUSINDIKA MAPARACHICHI.

Kusindika maparachichi kupata Guakamole.
Vifaa;-
  • • Mashine ya kusaga rojo
    • Bakuli ya kuoshea maparachichi
    • Kisu kikali kisichoshika kutu.
    • Chupa za kufungashia zenye mifuniko imara
    • Lebo
Malighafi;-
  • Maparachichi mawili
  • Kitunguu maji kimoja.
  • Pilipili kali moja.
  • Juisi ya limao kidogo.
  • Giligilani ya majani 25.
  • Chumvi na pilipili manga kidogo.
  • Maji safi na salama.
  • Nyanya moja kubwa.
Jinsi ya kutengeneza;-
  • • Menya kitunguu,
    • Kata kitunguu na pilipili kali,
    • Osha maparachichi na giligilani,
    • Saga giligilani kwenye mashine ya kusaga,
    • Ongeza maparachichi, juisi ya limao, nyanya, pilipili, kitunguumaji. Chumvi na pilipili manga,
    • Saga hadi mchanganyiko uwiane,
    • Fungasha guakamole kwenye chupa za kioo,
    • Weka lebo,
    • Hifadhi mahali penye baridi.
Matumizi;-
  • Hutumika kama sosi baridi pamoja na vitafunwa kam mikate au pamoja na mboga za majani.
  • Hutumika kama saladi (mchanganyiko wa matunda)
  • Hutumika ikiwa katika hali ya kusindikwa. Bidhaa inayotokana na parachichi ni “guakamole” ambayo hutumika pamoja na chipsi au chakula chochote kilichotengenezwa kutokana na nafaka.
VIRUTUBISHO.
Virutubishi vinavyopatikana kwenye gramu 100 za maparachichi
  • Maji gramu 72
  • Mafuta gramu 21.8
  • Wanga gramu 6
  • Nguvu kilokalori 875
  • Kalsiamu miligramu 10
  • Fosiforasi miligramu 34
  • Vitamini A I.U 800
  • Vitamini C miligramu 15

Saturday 20 August 2016

KILIMO BORA CHA KITUNGUU SAUMU

Kitunguu saumu ni moja kati ya zao bora lenye manufaa mengi kwa matumizi ya kila siku kwa maisha ya mwanadamu, kiafya, Kitabibu na kwaajili ya kutengeneza au kuchanganyia katika dawa tofauti. Pia ni kiungo mausui katika mambo ya mapishi.

Zipo aina tisa za kitunguu saumu ambazo hulimwa hapa duniani katika maeneo mbali mbali. Aina za kitunguu saumu maarufu kwa matumizi ya kawaida  ni tatu, ambazo ni;-

SOFT NECK---ni nyeupe huzaa kwa muda mfupi.

SILVER SKIN---vina rangi ya silver vikikaushwa vinauwezo wa kukaa hadi mwaka                                          mmoja.

ANTICHOKE---vina rangi nyekundu kwa mbali.
1.    Kitunguu saumu chenye mafuta makali
2.    Kitunguu saumu chenye madini ya protini
3.    Kitunguu saumu chenye madini , protini na mafuta mepesi.
Hiki ndicho tulacho kila siku hapa kwetu na wengi hutumia kama dawa wakati hakina sifa za kuwa dawa.

NAMNA YA KULIMA
Kitunguu hiki hulimwa maeneo yenye baridi, uwanda wa jua hafifu, mvua za wastani na joto hafifu, ardhi iwe nyeusi naa yenye rutuba na mfinyazi, kusiwe na upepo mkali au ukungu mwingi.
Hulimwa kwa kuandaa kitalu na kupandikizwa baada ya kufika urefu wa inchi 6-14, hupandwa kwa mstari na mche hadi mche ni nchi 3-4 na mstari kwa mstari ni nchi 12.
Kwa kifupi zao la kitunguu saumu ni gumu kulilima kwani hustawi katika maeneo machache sana hapa duniani . Kwa hapa Tanzania hustawi katika mkoa wa Manyara wilaya ya Mbulu, Hannang na Babati kidogo, Mkoa wa Kilimanjaro na kwa eneo lolote ambalo hali inaendana na maeneo tajwa hapo juu. Pia kwa Mkoa wa Morogoro vinalimwa maeneo ya Mgeta.

UANDAAJI WA SHAMBA

Tifua udongo kidogo kasha ufanye hallowing ili kurahisisha upandaji na ukaaji wa mimea tu. Tengeneza tatu za mita 1 hadi 1.5, upana mita 10 urefu. Kwa upande wa mbolea inashauriwa utumie WINNER.


UPANDIKIZAJI
Vibanguliwe na vipandwe kwa kuelekezea mizizi chini na kina cha wastani 2.5 inchi, mbolea ya samadi hushauriwa zaidi kutumika, huvunwa baada ya miezi 4-6 kulingana na hali ya hewa na aina ya hali ya mbegu iliyotumika.

SPACING/MUACHANO WA MBEGU NA MBEGU
Mstari hadi mstari ni inchi 8 na mmea hadi mmea ni inchi 6 yaani (8*6) inchi.

KIWANGO CHA MBEGU
Kiwango cha mbegu ni kilo 200-300 kwa heka moja.

MAVUNO
Mavuno ni tani 5 – 6 kwa heka moja.

UANDAAJI WA MBEGU
Kitunguu saumu hupandwa “BULB” na siyo mbegu kama vitunguu maji. Ni ile Punje ambayo imekuwa na kukomaa vizuri na isiyoathiriwa na magonjwa.

MAGONJWA
1.    Vitunguu saumu havishambuliwi na magonjwa kama ilivyo kwa mazao mengine.
2.    Mimea ikianza kutoa maua , yaache yawe marefu hadi yajikunje kisha utayakata ili kuongeza  uzalishaji.
Wadudu wasumbufu ni THRIPS na ukungu upande wa magonjwa.
Kwa upande wa ukungu anza na RIDOMILL GOLD upulizie mara nne kisha malizia na score kwaajili ya Thrips tumia ACTARA au MATCH.
Hushambuliwa na magonjwa kuanzia wiki ya tatu hadi ya saba, tumia madawa ya kupuliza yatumikayo kwa nyanya na vitunguu vya kawaida.

SOKO
Kwa Kariakoo kilo moja  ni kati ya shilingi 4000 – 6000. Ila kwa ujumla ni kati ya bidhaa ambayo inayohitajika kwa wingi ndani na nje ya nchi.
Tunakutakia kila lakheri katika safari yako ya Kilimo bora.

MAKALA HII IMEANDALIWA NA STANLEY NGOLE, MTAALAM WA MASUALA YA KILIMO.
Stanley Ngole,
+255 767 880 400,
shambani.kwetu.leo@gmail.com

Saturday 13 August 2016

Kilimo cha Mbaazi


Mbaazi ni zao jamii ya mikunde inayostawi katika nchi za kitropiki zenye mvua chache. Zao hili ni muhimu sana kwa nchi za Asia ambako ni mojawapo ya chakula kikuu hasa katika nchi ya India.

Kwa miaka ya hivi karibuni, zao la mbaazi limekuwa moja ya mazao muhimu ya biashara katika maeneo mengi ulimwenguni. Hii ni kutokana na ongezeko la walaji na uwezo wake wa kustahimili ukame na mvua chache ambao unaendana na mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni kote. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Manyara (Hanang na Mbulu), Arusha (Arusha vijijini na Meru), Dodoma (Kondoa), Kilimanjaro (Same, Mwanga, Rombo, Hai na Moshi vijijini) Mbaazi kwa kawaida hupandwa kwa msimu mmoja lakini aina za kienyeji zinaweza kulimwa kama zao la kudumu ambapo huweza kukaa shambani miaka mitatu hadi mitano ingawa uzalishaji wa mazao hupungua msimu hadi msimu.



Matumizi ya Mbaazi
Chakula/mboga hasa zikiwa mbichi. Mbaazi mbichi huwa na protini zaidi ya asilimia 21%, wanga asilimia 44.8%, mafuta asilimia 2.3% pamoja na baadhi ya virutubisho vya madini kama chokaa na chuma.
Zao la biashara. Kutokana na kuwepo kwa aina bora za mbaazi zinazohitajika kwa wingi katika soko la ndani na nje pamoja na kuwepo kwa aina zinazokomaa mapema na kuwahi soko la dunia, zao hili limekuwa likilimwa kwa ajili ya biashara hasa katika wilaya za Babati, Karatu, Arumeru pamoja na Kondoa
Chanzo cha nishati (kuni). Miti ya mbaazi hutumiwa kwa ajili ya kuni katika maeneo ya ukanda wa chini ambayo haina miti. Matumizi haya pia husaidia kupunguza uharibifu wa mazingira kutokana na watu kutokukata miti ovyo.
Kirutubisho cha udongo. Mbaazi ni jamii ya mikunde ambayo huongeza mbolea aina ya Naitrojeni kwenye udongo. Majani yake yanapopukutika na kudondoka ardhini huoza na kubadilika kuwa mbolea ambayo pia huboresha muundo wa udongo. Chakula cha mifugo. Maganda na majani ya mbaazi hutumika kama chakula kwa ajili ya kulishia mifugo.
Hali ya hewa
Mbaazi hustawi vizuri katika nyuzi joto 29 hadi 38, na hupandwa kuanzia usawa wa bahari hadi mita 1900 kutegemeana na aina ya mbegu. Kuna mbegu zinazostawi katika ukanda wa chini, wa kati na wa juu. Aidha kuna aina zinazostawi zaidi ya mita 2000 kutoka usawa wa bahari Zao hili huhitaji kiasi cha milimita 600 hadi 1000 cha mvua kwa mwaka. Aina za mbaazi za muda mfupi hutosha kustawi katika mvua kiasi cha milimita 250 hadi 370 kwa mwaka.
Udongo
Kwa kilimo chenye tija, ni vizuri kuotesha mbaazi kwenye udongo unaoruhusu maji, wenye mbolea kiasi na wenye tindikali kiasi cha pH kuanzia 5 hadi 7.



UTAYARISHAJI WA SHAMBA.
• Shamba la mbaazi litayarishwe mapema kwa kung’oa mabaki yote ya mimea pamoja visiki kabla ya kulilima.
• Lima shamba kiasi kisichopungua sentimeta 30.
• Lainisha udongo kwa kupitisha haro.
• Tayarisha matuta au makinga maji kama shamba liko kwenye mteremko.
Kuandaa mbegu
• Mbegu bora iliyochaguliwa vizuri na kuhakikiwa kiwango cha uotaji ziandaliwe.
• Mbegu ziwekewe dawa ya kuzuia kuvu (fungus) kabla ya kupanda ili kuzuia magonjwa yatokanayo na mbegu na udongo.
 Mbegu bora
Mbegu za mbaazi zimegawanyika katika makundi makubwa matatu nazo ni, mbegu za muda mfupi, mbegu za muda wa kati, mbegu za muda mrefu.

KUPANDA.
 1. Mbaazi za muda mfupi, zipandwe peke yake bila kuchanganya na mazao mengine. Nafasi: Kuwe na nafasi ya sentimeta 75 toka mstari na mstari, sentimita 20 toka shimo hadi shimo. Kiasi cha mbegu: Kilo 5 hadi 6 zaweza kutumika kwa ekari moja.

 2. Mbaazi za muda wa kati, zipandwe peke yake na katika mwinuko kutoka usawa wa bahari wa mita 1000 hadi 1880 Nafasi: Kuwe na nafasi ya sentimita 120 toka mstari hadi mstari na sentimita 30 toka shimo hadi shimo. Kiasi cha mbegu: Waweza kutumia kilo 5 kwa ekari moja.

3. Mbaazi za muda mrefu, zipandwe peke yake katika mwinuko toka usawa wa bahari wa mita 1000 hadi 1880. Nafasi: Kuwe na sentimita 150 toka mstari hadi mstari na sentimita 50 toka shimo hadi shimo. Kiasi cha mbegu: Waweza kutumia kilo 5 kwa ekari moja

PALIZI NA KUPUNGUZIA MIMEA.
Ni muhimu kupalilia mapema (angalau mara mbili kulingana na kiasi cha unyevu au mvua) na kuondoa magugu ambayo hushindana na mimea michanga. Miche ikiwa mingi kwenye shina husababisha mazao kuoza. Kwa hivyo ni muhimu kupunguza miche na kubaki miwili au kutegemeana na nafasi.

 WADUDU.
Kuna wadudu wa aina mbalimbali ambao kushambulia mbaazi, wakati zikiwa shambani au zikiwa galani.
1.       Vidukari
 Vidukari weusi wanaotembea kwa makundi na ambao huonekana zaidi katika sehemu changa za mimea kama vichomozo, matawi na majani. Wadudu hawa husambaa kwa wingi wakati wa majira ya ukame. Wadudu hawa hufyonza majimaji au utomvu ulio kwenye maeneo hayo na kusababisha mbaazi kubadilika rangi na kukauka. Udhibiti….Wadudu hawa hudhibitiwa kwa kutumia njia bora za kilimo na kufanya kilimo cha mzunguko.

2.       Kunguni wa mifuko ya mbaazi
 Kuna aina nne za wadudu hawa ambao ni Kunguni wa kahawia (Claiigralla spp), Kunguni wakubwa (Anoploenemies spp), Riptutasi (Riptortus dentipes), Kunguni wa kijani (Nezara viridula). Wadudu hawa hufyonza mbegu inayokuwa kupitia kuta za mifuko na kufanya mbegu kuoza na kukosa thamani ya kuwa mbegu na chakula cha binadamu. Udhibiti….Wadudu wanaofyonza mifuko ni vigumu kuwadhibiti kwani huruka kutoka sehemu moja na kwenda nyingine hivyo wanaweza kukusanywa kwa chandarua na kuangamizwa.

3.       Mbawakavu wa maua na chavua (Blister beetles)
 Wadudu hawa wenye rangi ya njano hula maua na kupunguza uzalishaji wa mifuko ya mbaazi. Katika eneo ambalo uzalishaji wa mbaazi ni mkubwa, wadudu hawa hufanya uharibifu mdogo kuliko katika eneo ambalo mbaazi huzalishwa kwa kiasi kidogo. Udhibiti….Wadudu hawa wanaweza kudhibitiwa kwa kuwaondoa kwa mikono na kuwauwa isipokuwa wakati wa kuwashika kuwepo na uangalifu kwani wakisumbuliwa huweza kutoa kemikali ambayo inaweza kuunguza mikono au mwili.

4.       Funza wa vitumba (Maruca vitrata)
Wadudu hawa hutaga mayai kwenye vikonyo vya mbaazi kabla ya kuchanua au juu ya mifuko hula vikonyo vya maua na mbegu iliyoko ndani ya mifuko ya mbaazi. Udhibiti….Mkulima anaweza kuwadhibiti wadudu hawa kwa kufanya ukaguzi wa shamba mara kwa mara ili kufahamu uwepo wa wadudu hawa, pamoja na kutumia viuatilifu kulingana na maelekezo ya mtaalamu wa kilimo. Ni vyema ukaguzi ukafanyika wiki moja kabla ya mbaazi kuchanua na baada.

5.       Inzi wa mifuko (Melanagromyza chacosoma)
Hawa ni wadudu wadogo weusi warukao na wanaotaga mayai katika kuta za mifuko za mbaazi inavyokua. Funza wake ni weupe na wana urefu wa sentimeta 3. Wadudu hawa hufanya uharibifu mkubwa kwa kula mbegu changa iliyopo kwenye mifuko. Udhibiti….Katika maeneo ambayo wadudu warukao ni tatizo, jamii ya mikunde inayokomaa kwa muda tofauti isipandwe kwenye shamba moja ili kuzuia mwendelezo wa kuzaliwa kwa inzi hawa hasa kila aina ya mikunde inapotoa maua. Pia mwarobaini waweza kunyunyiziwa mara 4 kila baada ya wiki kwa kiwango cha gramu 50.

6.       Vithiripi (Megalurothrips spp. And Frankliniella schultzei)
Wadudu hawa wadogo na wenye rangi ya kahawia na mabawa ya njano huathiri mbaazi hasa kwa kufyonza utomvu kwenye majani na maua.Husababisha maua na vikonyo kusinyaa, kufifia rangi na kudondoka kabla ya kukomaa. Udhibiti….Kagua shamba kila mara ili kufahamu uwepo wa wadudu hao kabla ya mimea kuchanua ili kudhibiti mapema.

7.        Vipekeche
 Hawa ni wadudu wanaoshambulia mbaazi ikiwa ghalani. Wadudu hawa hutoboa mbegu na kutengeneza mashimo ya kutokea wadudu kamili.

IFAHAMU TANGAWIZI NA SOKO LAKE


Kwa ujumla tangawizi hustawi kwenye mwinuko kuanzia m 800 mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari, kwa ujumla maeneo mengi inakostawi kahawa na tangawizi zinastawi.

KUANDAA SHAMBA
Andaa Shamba lako mapema, katua/lima kuanzia miezi ya
April, may au June, ni vizuri ukaanzisha Shamba jipya au lilikaa bila kulimwa kwa miaka mitatu, Lainisha udongo miezi ya August au September na kuanzia November unaweza kuanza kupanda.
.
KUPANDA
Tangawizi hupandwa kwa kuivunja vunja kwa kufuatisha mbingili zake. Panda tangawiz kwa cm 30 kati ya shina moja na jingine na cm 45 mpaka 60 kati ya mstari mmoja na mwingine. Tumia  mbolea ya mboji au samadi na usitumie  mbolea za kemikali kupandia, Kg 1000 za tangawiz hupandwa katika hekta moja na unaweza kuvuna kuanzia tani 10 mpaka 25 inategemea ukubwa wa mbegu, urutubishaji, kiasi cha maji na paliz. Huchukua wiki mbili mpaka mwezi mmoja na nusu tngwz Kuota inategemea kiasi cha maji na joto kwenye udongo, ni vizuri kuzitandaza tangawz kwenye kivuli na kufunika na gunia na kuzimwagilia ili ziote kabla hujazikataka kwa ajili ya kwenda kupanda. Palilia Mara  Majani yanaoota na pandishia udongo kwenye mashina ili tangawiz itanuke vizuri.

MAGONJWA
Tangawiz haishambuliw sana na magonjwa ila Mara chache hushambuliwa na kuvu (fungus).

Mkulima ameshika shina moja la Tangawizi lenye zaidi ya Kg 1
KUVUNA
Huchukua miez 6 mpaka 18 mpaka kukomaa inategemea mwinuko toka usawa wa bahar na mvua.
 Tangawiz haitaki maji yanayotuama kama vijaruba vya mpunga, maji yakituama kwenye shina la tangawiz kwa mda Fulani Majani ya tangawiz huwa ya njano na huanza kunyauka

 Kuvuna Tani 10 kwa hekta moja ni kadirio la chini kabisa.. Kipindi soko linapokua zuri unaweza kupata kuanzia Mil 20 mpaka 60 kwa hekta moja, kuna wahindi ambao hununua tangawizi kwa wingi sana na wanaexport, wahindi hununua kg 1 kwa sh 3000, mpaka 3500 ukiuzia shambani
Uzuri tangawizi unaweza kusubir soko zuri na ukauza kwa bei nzuri kwani zao hili hupanda bei haraka

Watu wengi wanashindwa kuzalisha tangawizi kwa wingi kwa kukosa mitaji ya kununulia mbegu kwani mbegu zake ni gharama, hivyo unashauriwa kununua kg chache walau kg 200 ukapanda eneo Dogo ili kuzĂ lisha mbegu ambazo utaweza kuzisambaza eneo kubwa, na kwa kulima eneo Dogo unaweza kupata  uzoefu kupitia hapo na kujua kama  eneo ulilolima ni sahihi na linafaa kwa kilimo cha tangawiz.

 Sokoni tangawiz huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri, pia tangawz kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg.
 Usikatishe tamaa pale  tangwizi inashuka bei mpaka sh. 1500, unaweza kusubir kwa mda mfupi na kuuza tangawiz kwa bei nzuri sana kwa kua bei yake huwa hupanda kwa haraka.

Mkulima wa Tangawizi Songea

HALI YA HEWA
Mimea hii husitawi katika maeneo  yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu.  Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi.  Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota

Mvua:  kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo

Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile  haihitaji udongo wenye  kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0.

 Jamani tusiogope kuwekeza, na kujaribu fursa mpya, Nina imani nimeeleweka na karibuni kama kuna maswali..

Wednesday 3 August 2016

Jinsi ya kutengeneza Chilli Sauce


Unaweza kuwa Mjasilia mali kwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya fursa moja tu kati ya nyingi ambazo unakutana nazo katika maisha yako ya kila siku. Leo nmekuletea makala ya namna ya kutengeneza Chilli Sauce. Fuatilia makala hii ukapate kujikwamua kwa namna moja ama nyingine kuzidi kuutokomeza umasikini kwenye jamii zetu.

Yafutayo ndiyo mahitaji kwa ajili ya kutengenezea chili souce;

a) Pilipili mbuzi nyekundu robo 1/4 kilo.

b) Nyanya kilo moja.

c) Kitunguu swaumu kikubwa kimoja.

d) Mafuta ya kula vijiko 7 vya chakula.

e) sukari vijiko viwili vya chai.

f)  maji ya moto kikombe kimoja cha chai.


g) vinega vijiko 3 vya chai.

Baada ya kuandaa mahitaji hayo ya jinsi ya kutengeneza chili souce, twende kuona moja kwa moja jinsi ya kutengeneza chili souce.

HATUA YA KWANZA.

-Kata Pilipili kuondoa mbegu.

-menya nyanya kuondoa mbegu pia.

-menya vitunguu swaumu kisha vikatekate viwe katika vipande vidogo vidogo.

NB; baada ya kumaliza hatua hiyo ya maandalizi chukua Brenda, kisha saga mchanganyiko wote wa malighafi ambazo nimezianisha kwenye hatua ya kwanza. Saga mchanganyiko huu mpaka uone imetoka rojo laini.

HATUA YA PILI.

Ukishamaliza kusaga mchanganyiko huu hapo juu jambo ambalo unatakiwa kulifanya ni;

*Chukua sufuria yenye nafasi ya kutosha kwa ajili ya kupika mseto huu.

*Weka sufuria yako jikoni, iache kwa sekunde kadhaa ili ipate moto pia kama kuna maji katika sufuria yaweze kukauka.

*Baada ya kuona sufuria yako imekwisha kupata moto, chukua mafuta ya kula yaweke kwenye sufuria, yaache yachemke.

* mafuta yakichemka chukua mseto wako mwagia katika sufuria yako, koroga mseto huo kuelekea upande mmoja kwa dakika 30 huku mseto huo ukiendelea kuchemka.

* Baada ya dakika 30 epua mseto huo na uuache upoe, kisha funga katika vifungashio kwani mseto huo utakuwa umeshakuwa chili souce.

Mpaka kufikia hapo utakuwa umekwisha kutengeneza  chili souce ambayo inafaa kwa ajili ya matumizi ya binadamu kwani ni salama kwa ajili ya afya yetu.

Strawberry: Tunda mwitu lenya faida kubwa


Zao hili hustawi katika joto la wastani, na hukua kwa haraka zaidi na uzalishaji kuongezeka linapolimwa kisasa, hasa katika nyumba maalumu ya kuzalishia mimea yaani green house. Zao hili hukua vizuri katika mwinuko wa mita 1500 kutoka usawa wa bahari. Endapo unahitaji kuzalisha stroberi  katika maeneo ya bondeni itakulazimu kuwa na maji kwa wingi kwa ajili ya umwagiliaji wa mara kwa mara.

Udongo
Stroberi inaweza kustawi vizuri kwenye udongo tifutifu wenye rutuba. Zao hili haliwezi kustahimili ukuaji kwenye udongo wenye chachu nyingi, hasa chokaa kwani mizizi yake huoza kwa urahisi.

Kupanda
Ili kuwa na mazao bora ambayo yatakuwezesha kupata soko la uhakika, bila vipingamizi, inashauriwa kuzalisha kwenye nyumba maalumu ya kuzalishia mazao (green house). Katika kuzalisha stroberi baada ya kujenga green house andaa mabomba ya plastiki ambayo yatawezesha kutoboa matundu kwa urahisi (tazama picha).
• Matundu katika bomba hilo yawe na umbali wa inchi 1.
• Ni vyema matundu hayo yakawa zigizaga, ili kuruhusu mimea utakayopanda kukua vizuri bila kuwekeana kivuli.
• Tandika karatasi la nailoni sakafuni ili kuwezesha maji utakayotumia kunyeshea kurudi kwenye bwawa au sehemu ya kuhifadhia.
• Ning’iniza mabomba hayo kwa kutumia waya.
• Jaza kokoto, yenye mapande makubwa kiasi.
• Panda miche kwenye kila tundu kwa uangalifu ili mizizi isikatwe na kokoto zinazoshikilia mmea.

Kumwagilia
Mimea ya stroberi inahitaji maji kwa kiasi kikubwa sana. Hii inamaanisha kuwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa umwagiliaji kabla ya kuanza kilimo cha zao hili. Unapaswa kumwagilia mara nne kwa siku, kila baada ya saa nne unapaswa kumwagilia kwa robo saa. Hii itawezesha mimea yote kupata maji ya kutosha. Endapo stroberi haitapata maji ya kutosha, uzalishaji wake pia utakuwa ni hafifu sana, kwani maua hayatachanua ipasavyo na hata matunda kukomaa inakuwa ni shida.

Mbolea
Uzalishaji wa kisasa wa stroberi, unaambatana na ufugaji wa samaki kwenye bwawa ndani ya green house. Mbinu hii husaidia mimea kupata mbolea inayotokana na chakula wanacholishwa samaki kwenye bwawa, kwani maji yanayofugia samaki ndiyo hayo yanayotumika katika mzunguko wa umwagiliaji. Hii inamaanisha kuwa hakuna mbolea nyingine inayohitajika kwa ajili ya stroberi.

Wadudu na magonjwa
Endapo stroberi inazalishwa kwenye nyumba maalumu ya mimea, hakuna magonjwa wala wadudu wanaoishambulia. Ikiwa mkulima anazalisha stroberi kwenye eneo la wazi, stroberi inaweza kushambuliwa na magonjwa ya ukungu, pamoja na magonjwa yanayosababishwa na virusi.

Dawa
Endapo stroberi itashambuliwa na magonjwa ya ukungu na virusi, nyunyizia dawa za asili kama vile pareto na mwarobaini, na baada ya muda kutakuwa na matokeo mazuri.

Kuvuna
Zao la stroberi, huzaliana na kukomaa kwa haraka sana. Unaweza kuanza kuvuna stroberi baada ya mwezi mmoja tangu kupandwa. Kila wiki stroberi inakuwa na matunda mapya, na kila tunda likishatokeza huiva kwa haraka, hivyo uvunaji wake ni wa mfululizo. Ikishafikia hatua hiyo tegemea kuwa na wiki 2-3 za kuvuna mfululizo. Kwa kuwa matunda ya stroberi ni laini, epuka kushika tunda wakati wa uvunaji ili lisiharibike. Shika kikonyo cha tunda ili kuvuna kwa usalama. Usiache matunda yaliyoiva shambani kwa muda mrefu kwani yanaweza kusababisha mimea kuoza. Pia yatapoteza ladha na virutubisho halisi vinavyotakiwa.

Virutubisho

Stroberi ina kiasi kikubwa cha virutubisho hasa vitamin B, C, K, na E . Pia yana wingi wa madini ya chumvi. Matunda haya husaidia kuchangamsha mwili na yana kiasi kidogo cha kalori.


Matumizi ya stroberi
Matunda ya stroberi yana matumizi mbalimbali kulingana na uhitaji wa mtumiaji, jamii na maeneo. Miongoni mwa matumizi hayo ni pamoja na:
• Kuliwa kama tunda.
• Kutia ladha katika aina mbalimbali za vyakula.
• Kuweka rangi, harufu na nakshi katika vipodozi.
• Kutengeneza marashi n.k.

Soko na bei
Stroberi ina soko zuri kulingana na ubora wake. Kwa sasa gramu 50 za stroberi zinauzwa kati ya shilingi 5,000-10,000 za kitanzania.

Friday 29 July 2016

Kilimo cha Pilipili



(iii) PILIPILI
Pilipili ni kiungo kikali, hutumiwa kwa kukoleza mchuzi na vyakula mbali mbali. Pilipili zinaweza kupikwa zikiwa nzima au kukatwakatwa na kutumiwa katika kachumbari; au kuwekwa kwenye siki na achali, au kusagwa na kutumia unga wake.
Hili ni zao la nchi za kitropiki, na hutumiwa sana na wakazi wa Bara Hindi, Mashariki ya Mbali. Amerika ya Kusini na Afrika ya Tropiki. Pilipili huwekwa katika makundi makubwa mawili, yaani: 
1. Pilipili Hoho (Hot Pepper)- Hizi ni ndogo ndogo, ndefu, nyembamba, na kali sana. Aina zinazojulikana zaidi ni Green Chilli, Cherry Pepper, Long Cayenne na Tabasco.

2. Pilipili Manga (Sweet Pepper)- Hizi zina umbo kubwa, nyama nying, mviringo na ndefu kidogo, siyo kali. Aina zinazojulikana zaidi ni Sweet, Neapolitan, Keystone, Giant, Ynlo Wonder na california wonder.
Kupanda: Mbegu hupandwa kwenye kitalu ambamo hukaa kwa muda wa majuma manane hadi kumi. Kisha miche hupandikizwa bustani kwa umbali wa sentimeta 45 kwa 90.
Kuvuna: Umri wa kuvuna zao hili hutegemea aina ya pilipili na matumizi yake. Aina ambayo ni kubwa na tamu kwa kawaida huvunwa kabla haijapevuka na kugeuka rangi yake. Pilipili katika hali hii hutumiwa zaidi kwenye michuzi, kachumbali na kutiwa kwenye makopo. 
Pilipili kali, ambayo mara nyingi ni ndogo ndogo, kwa kawaida huvunwa baada ya kupevuka na kuwa nyekundu. Halafu hutumiwa katika mapishi na vyakula mbali mbali, lakini sehemu kubwa zaidi hukaushwa na kusagwa ili kupata unga wake.

Magonjwa: Damping- off, Bacteria Spot, Fusarium wilt na Antracnose, ni miongoni mwa magonjwa yashambuliayo zao hili. Tuseme magonjwa ya pilipili ni sawa na ya Nyanya. Hivyo njia za kupigana nayo ni sawa.
Wadudu: Wadudu ambao hushambulia zao hi wengi, lakini walio wabaya zaidi ni Aphids, Cut worm, Flea beetle, Pepper weevil na Pepper Maggot.
Kinga: Parathion 1% au Chlrdane 5%. Dawa itumiwe mara wadudu watokeapo na kurudiwa kila baada ya siku 7.
Ahsanteni!