Wednesday 3 August 2016

Jinsi ya kutengeneza Chilli Sauce


Unaweza kuwa Mjasilia mali kwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya fursa moja tu kati ya nyingi ambazo unakutana nazo katika maisha yako ya kila siku. Leo nmekuletea makala ya namna ya kutengeneza Chilli Sauce. Fuatilia makala hii ukapate kujikwamua kwa namna moja ama nyingine kuzidi kuutokomeza umasikini kwenye jamii zetu.

Yafutayo ndiyo mahitaji kwa ajili ya kutengenezea chili souce;

a) Pilipili mbuzi nyekundu robo 1/4 kilo.

b) Nyanya kilo moja.

c) Kitunguu swaumu kikubwa kimoja.

d) Mafuta ya kula vijiko 7 vya chakula.

e) sukari vijiko viwili vya chai.

f)  maji ya moto kikombe kimoja cha chai.


g) vinega vijiko 3 vya chai.

Baada ya kuandaa mahitaji hayo ya jinsi ya kutengeneza chili souce, twende kuona moja kwa moja jinsi ya kutengeneza chili souce.

HATUA YA KWANZA.

-Kata Pilipili kuondoa mbegu.

-menya nyanya kuondoa mbegu pia.

-menya vitunguu swaumu kisha vikatekate viwe katika vipande vidogo vidogo.

NB; baada ya kumaliza hatua hiyo ya maandalizi chukua Brenda, kisha saga mchanganyiko wote wa malighafi ambazo nimezianisha kwenye hatua ya kwanza. Saga mchanganyiko huu mpaka uone imetoka rojo laini.

HATUA YA PILI.

Ukishamaliza kusaga mchanganyiko huu hapo juu jambo ambalo unatakiwa kulifanya ni;

*Chukua sufuria yenye nafasi ya kutosha kwa ajili ya kupika mseto huu.

*Weka sufuria yako jikoni, iache kwa sekunde kadhaa ili ipate moto pia kama kuna maji katika sufuria yaweze kukauka.

*Baada ya kuona sufuria yako imekwisha kupata moto, chukua mafuta ya kula yaweke kwenye sufuria, yaache yachemke.

* mafuta yakichemka chukua mseto wako mwagia katika sufuria yako, koroga mseto huo kuelekea upande mmoja kwa dakika 30 huku mseto huo ukiendelea kuchemka.

* Baada ya dakika 30 epua mseto huo na uuache upoe, kisha funga katika vifungashio kwani mseto huo utakuwa umeshakuwa chili souce.

Mpaka kufikia hapo utakuwa umekwisha kutengeneza  chili souce ambayo inafaa kwa ajili ya matumizi ya binadamu kwani ni salama kwa ajili ya afya yetu.

No comments:

Post a Comment