Kitunguu
saumu ni moja kati ya zao bora lenye manufaa mengi kwa matumizi ya kila siku
kwa maisha ya mwanadamu, kiafya, Kitabibu na kwaajili ya kutengeneza au
kuchanganyia katika dawa tofauti. Pia ni kiungo mausui katika mambo ya mapishi.
Zipo
aina tisa za kitunguu saumu ambazo hulimwa hapa duniani katika maeneo mbali
mbali. Aina za kitunguu saumu maarufu kwa matumizi ya
kawaida ni tatu, ambazo ni;-
SOFT
NECK---ni nyeupe
huzaa kwa muda mfupi.
SILVER
SKIN---vina rangi ya
silver vikikaushwa vinauwezo wa kukaa hadi mwaka mmoja.
ANTICHOKE---vina rangi nyekundu kwa mbali.
1.
Kitunguu
saumu chenye mafuta makali
2.
Kitunguu
saumu chenye madini ya protini
3.
Kitunguu
saumu chenye madini , protini na mafuta mepesi.
Hiki ndicho
tulacho kila siku hapa kwetu na wengi hutumia kama dawa wakati hakina sifa za
kuwa dawa.
NAMNA YA KULIMA
Kitunguu
hiki hulimwa maeneo yenye baridi, uwanda wa jua hafifu, mvua za wastani na joto
hafifu, ardhi iwe nyeusi naa yenye rutuba na mfinyazi, kusiwe na upepo mkali au
ukungu mwingi.
Hulimwa
kwa kuandaa kitalu na kupandikizwa baada ya kufika urefu wa inchi 6-14, hupandwa
kwa mstari na mche hadi mche ni nchi 3-4 na mstari kwa mstari ni nchi 12.
Kwa
kifupi zao la kitunguu saumu ni gumu kulilima kwani hustawi katika maeneo
machache sana hapa duniani . Kwa hapa Tanzania hustawi katika mkoa wa Manyara
wilaya ya Mbulu, Hannang na Babati kidogo, Mkoa wa Kilimanjaro na kwa eneo
lolote ambalo hali inaendana na maeneo tajwa hapo juu. Pia kwa Mkoa wa Morogoro
vinalimwa maeneo ya Mgeta.
UANDAAJI WA SHAMBA
Tifua
udongo kidogo kasha ufanye hallowing ili kurahisisha upandaji na ukaaji wa
mimea tu. Tengeneza tatu za mita 1 hadi 1.5, upana mita 10 urefu. Kwa upande wa
mbolea inashauriwa utumie WINNER.
UPANDIKIZAJI
Vibanguliwe
na vipandwe kwa kuelekezea mizizi chini na kina cha wastani 2.5 inchi, mbolea
ya samadi hushauriwa zaidi kutumika, huvunwa baada ya miezi 4-6 kulingana na
hali ya hewa na aina ya hali ya mbegu iliyotumika.
SPACING/MUACHANO WA
MBEGU NA MBEGU
Mstari
hadi mstari ni inchi 8 na mmea hadi mmea ni inchi 6 yaani (8*6) inchi.
KIWANGO CHA MBEGU
Kiwango
cha mbegu ni kilo 200-300 kwa heka moja.
MAVUNO
Mavuno
ni tani 5 – 6 kwa heka moja.
UANDAAJI WA MBEGU
Kitunguu
saumu hupandwa “BULB” na siyo mbegu kama vitunguu maji. Ni ile Punje ambayo
imekuwa na kukomaa vizuri na isiyoathiriwa na magonjwa.
MAGONJWA
1. Vitunguu saumu havishambuliwi na
magonjwa kama ilivyo kwa mazao mengine.
2. Mimea ikianza kutoa maua , yaache yawe
marefu hadi yajikunje kisha utayakata ili kuongeza uzalishaji.
Wadudu
wasumbufu ni THRIPS na ukungu upande wa magonjwa.
Kwa
upande wa ukungu anza na RIDOMILL GOLD upulizie mara nne kisha malizia na score
kwaajili ya Thrips tumia ACTARA au MATCH.
Hushambuliwa
na magonjwa kuanzia wiki ya tatu hadi ya saba, tumia madawa ya kupuliza
yatumikayo kwa nyanya na vitunguu vya kawaida.
SOKO
Kwa
Kariakoo kilo moja ni kati ya shilingi
4000 – 6000. Ila kwa ujumla ni kati ya bidhaa ambayo inayohitajika kwa wingi
ndani na nje ya nchi.
Tunakutakia
kila lakheri katika safari yako ya Kilimo bora.
MAKALA
HII IMEANDALIWA NA STANLEY NGOLE, MTAALAM WA MASUALA YA KILIMO.
Stanley
Ngole,
+255
767 880 400,
shambani.kwetu.leo@gmail.com
No comments:
Post a Comment