Sunday, 24 July 2016

FAHAMU ZAIDI KUHUSU MLONGE


Mlonge au moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean. Mti huu umeripotiwa kutibu zaidi ya magonjwa 300 ikiwemo magonjwa mbalimbali sugu.

Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa. Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.

Mbegu za mlonge zimekuwa dili kubwa duniani kwa sasa, zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Marekani na China na kwa mujibu wa taarifa ni kuwa zinauzwa mpaka 45000 ya Tanzania kwa gramu 500. Walikuja pia wachina kuzinunua kwa wingi na walikuwepo hapa bei ya mbegu za mlonge ilifika mpaka 11000 kwa kg kwa bei ya jumla yaani kwa anayechukua kg 100 au 500 au 1000 na kwenda juu. Taarifa zisizo rasmi zinadai wachinja hawa walikimbia nchini baada ya serikali kuanza kufuatilia na kuwakamata wakwepaji kodi bandarini. Isingekuwa hivi mpaka leo mlonge ungekuwa umeshatowka wote Tanzania.


Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani. Kile ulikuwa hujui ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajioli ya binadamu na wanyama.

Mlonge una:

Kalsiumu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe

Potasiamu mara 15 zaidi ya ile ya kwenye ndizi

Una vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti

Una protini nyingi mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi

Una klorpfiti (kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea) mara 4 zaidi ya ile ya kwenye nyasi au majani ya ngano (wheatgrass)

Una madini chuma mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach

Una vitamini A mpaka Z

Una omega 3, 6 na 9

Una asidi amino zile muhimu zinazohitajika na mwili

Una kiasi cha kutosha cha madini ya zinc ambayo ni madini muhimu katika kuongeza homoni za kiume na nguvu za kiume kwa ujumla

Mlonge ndicho chakula chenye afya zaidi juu ya ardhi:

Mlonge una jumla ya virutubishi 92, mmea au mti mwingine wenye virutubishi vingi basda ya mlonge una virutubishi 28. Mlonge una vionsa suku 46 na viondoa uvimbe mbalimbali mwilini 36, una asidi amino 18 na asidi amino muhimu zaidi 9 ambazo miili yetu haina uwezo wa kuzitengeneza.

Unga wa majani ya mlonge unao uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya 300 mwilini, magonjwa hayo ni pamoja na :

1. HUko Afrika magharibi madaktari hutumia mlonge kutibu kisukari.

2. HUko India mlonge hutumika kutibu shinikizo la juu la damu

3. HUtibu matatizo u maumivu ya mishipa

4. Hutuliza mapigo ya juu ya moyo

5. Hutibu kansa

6. Pumu

7. Hutuliza wasiwasi

8. Kikohozi

9. Maumivu ya kichwa

10. Inazuia na kushusha ile lehemu hata ile ya juu zaidi

11. Inapunguza mafuta tumboni

12. Inaweza sawa homoni

13. Inatibu maumivu wakati wa hedhi

14. Unasafisha ini

15. Inasafisha mkojo na kibofu cha mkojo

16. Inarekebisha matatizo kwenye tezi

17. Unatibu kipindupindu na kuharisha

18. Kifua kikuu

19. Kichwa kizito

20. Uchovu

21. Mzio

22. Vidonda vya tumbo

23. Maambukizi kwenye ngozi

24. Maumivu mbalimbali mwilini

25. Huondoa madoa doa meusi kwenye ngozi

26. Husafisha damu

27. Hutibu matatizo kwenye koo

28. Huondoa makohozi mazito kooni

29. Huondoa taka na msongamano kifuani

30. Hutibu kipindipindu

31. Huondoa moto wa jicho au uvimbe kwenye jicho

32. Hutibu maambukizi kwenye macho na kwenye masikio

33. Unatibu homa

34. Maumivu kwenye maungio

35. Huondoa chunusi

36. Hutibu matatizo karibu yote ya ngozi na kinga ya mwili

37. Matatizo kwenye mfumo wa upumuaji

38. Inatibu kiseyeye

39. Huongeza uwingi wa mbegu za kiume na nguvu kwa ujumla

40. Inatibu minyoo

41. Huongeza maziwa kwa wingi kwa mama anayenyonyesha

42. Huondoa uvimbe kwenye utumbo mpana

43. Inatibu ugonjwa wa kuvimba mwili

44. Inatibu kuhara damu

45. Inatibu kisonono

46. Unatibu tatizo la kukosa usingizi

47. Unatibu homa ya manjano

48. Unatibu malaria

49. Unatibu U.T.I na matatizo mengine kwenye mfumo wa mkojo

50. Unasaidia pia kujenga na kuimarisha misuli

51. Unatibu magonjwa ya mifupa

Mlonge uansafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele. Wakati unatumia mlonge unakufanya ujisikie vizuri, ujisikie mpya na mwenye nguvu. Watu wengi wanaotumia mlonge huwa ni wenye afya nzuri hata kwa muonekano tu hata wanapokuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 90.

Majani ya mti wa mlonge pia yanaweza kutumika kutengeneza biogas. Hutumika pia kama chakala cha wanyama kama sungura , mbuzi, ng’mbe. Mbwa n.k. Sungura wanaonekana kupenda zaidi mlonge kuliko wanyama wote.

Wednesday, 20 July 2016

KILIMO BORA CHA APPLE "MATUFAA"




Tufaa ni tunda moja maarufu duniani ambalo hupendwa kuliwa na watu wa jamii zote, hii inatokana na utamu wake pamoja na faida za kiafya zinazopatikana kwa kula matufaa. Matunda haya hustawi zaidi kwenye nyanda za juu ambako joto sio kali, sehemu kama lushoto, Arusha, miteremko ya Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Njombe, Songea nk. Udongo ni wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji.
Unaweza kupanda kwa kutumia mbegu au kwa kununua miche bora kutoka kwenye taasisiza kilimo mfano Uyole Mbeya. kama utatumia mbegu basi ni bora kununua mbegu bora au ukikosa mbegu basi jaribu kutumia zile utakazopata kutoka kwenye tunda lenyewe

Kama utachukua za kwenye tunda basi zikaushe kwenye jua kwanza mpaka zikauke kabisa, zile za kukununua huwa zimekauka kwa hiyo huna haja ya kuzikausha, Chukua karatasi laini (napkins/tissues) iloweshe maji kiasi kidogo kisha chukua mbegu zako na uzifunge na  karatasi hii vizuri kisha ziwekw kwenye jokofu kwa kiasi cha wiki 3-4 zitaanza kuota/kumea, kuziweka kwenye friji husaidia kuua vijidudu vya magonjwa ambavyo huenda vilikuwepo kwenye tunda au mbegu

Chukua mbegu yako na uipande kwenye mifuko au chombo kama ndoo, usipande kwenye vifuko vidogo maana mmea huu hukua mkubwa kiasi na wenye mizizi mikubwa kabla ya kupandwa. Mmea wako ukifikia ukubwa wa futi moja mpaka pili ni kipindi kizuri kuuhamishia shambani,

Umbali wa shimo hadi shimo ni kiasi cha futi 15 mpaka 18 kutoka mti hadi mti. Hakikisha unapanda miche yako wakati wa mvua za kwanza, Mashimo yawe na kina cha futi mbili na upana futi 3. Weka kasi cha debe 1 la samadi au mboji na changanya vizuri na udongo.



kumbuka kuacha kisahani kwa ajili ya kukusanya maji ya mvua au unapomwagilia na utandaze majani/nyasi kiasi cha futi 3 kuzunguka mti wako, hakikisha wanyama kama mbuzi na ng'ombe hawaingii shambani na kula miti yako. Baada ya mwaka hutakuwa tena na haja ya kumwagilia miti yako kwani itaweza kukua yenyewe kwa kutegemea mvua

WADUDU NA MAGONJWA
Wadudu wanaoshambulia zaidi mitufaa ni vidukari (moth) na pia ugonjwa wa madoa meusi (black spot) ndio unaoshambulia zaidi, ili kupambana na ugonjwa na wadudu hawa hakikisha unatuma kiutilifu chochote che nye pareto (pyrethrum) ndani yake.

KUVUNA
Uvunaji ni baada ya miaka mitatu lakini miche ya kuunga huanza kuzaa mapema hata ndani ya mwaka, ila nashauri usiruhusu matunda mengi kwenye miti midogo ili kuzuia matawi kuvunjika kwa hiyo punguza matunda kabla hayajawa makubwa na kubakisha machache.

KILIMO BORA CHA NANASI



Zao la mananasi hulimwa sana hapa nchini maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Geita, Mwanza, Tanga, MtwaraLindi na maeneo mengine. Zao hili lina kiasi kikubwa cha vitamini A na B na kiasi kidogo cha vitamini C, pia kuna madini kama potasiam, kalsiam, chuma na magnesiam.

HALI YA HEWA
Manansi hustawi sana ukanda wa pwani usawa usiozini mita 900 toka usawa wa bahari ambapo kuna mvua nyingi kiasi cha milimita 1500 na unyevu wa kutosha, pia unaweza kupanda kwenye maeneo yenye mvua chache lakini kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, Hali ya joto ni kuanzia sentigredi 15 - 32, huwa haya stahimili baridi

UDONGO
Udongo wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji ndi unaofaa kwa ajili ya kilimo cha mananasi, unaweza kutumia samadi au mbole vunde ili kuongezea rutuba ya udongo wako. 

MSIMU
Kwa ukanda wa pwani wenye mvua mbili kwa mwaka upandaji wa mananasi huanza mara baada ya mvua za kwanza kuanza, ni vizuri kupanda kwa muda mfupi ili uzaaji usipishane sana na pia kusaidia kupata mvua za kutosha kabla ya msimu kuisha.

UPANDAJI
Tumia miche ya aina moja na yenye umri sawa ili huduma zifanane na pia uzaaji uwe wa mpangilio, umbali toka mmea hadi mmea ni sentimeta 30 na mstari hadi mstari ni sentimeta 60, na umbali kila baada ya mistari miwili miwili ni sentimeta 90.



Kwa ekari moja unaweza kupanda miche 25,200 na kwa hekta moja unaweza kupanda miche 44,000. ili mananasi yako yastawi vizuri basi tengeneza kama mtaro mdogo na kwenye mitaro ndio upande mananasi yako, hii husaidia kupata unyevu zaidi 

MBOLEA
Kwa wale wanaotumia mbolea za viwandani, ni vizuri kutumia NPK na DAP ambazo utaweka miezi miwili baada ya kupanda na miezi 12 baada ya kupanda baada ya hapo hautahitaji mbolea tena, lakini ni vizuri zaidi kama utatumia mbolea za asili

WADUDU
Wadudu wanaoshambulia mananasi ni aina ya mealybug ambao huondolewa kwa kupulizia dawa kama dume na karate.



Ugonjwa wa kuoza moyo wa miche unaweza kuzuiwa kwa kupiga dawa za copper oxychloride au kwa kuzamisha miche kwenye dawa za fungasi (fungicides)kabla ya kupandwa shambani

UVUNAJI
Mananasi huwa tayari kuvunwa miezi 18  mpaka 24 baada ya kupandwa kutegemeana na mbegu na matunzo ikiwemo kiasi cha mvua, mbolea na unyevu shambani, Uvunaji  hufanyika kwa kutumia visu na vibebeo maalum kuhakikisha ubora wa zao hili.


UMUHIMU WA MAJIVU KWENYE UDONGO WA BUSTANI.



Watu wengi wamekuwa wakiulizia umuhimu wa madini kwenye udongo na namna ya asili ya kuongezea kosefu wa madini kama potasiam, fosforas, kalsiam na mengineyo, njia rahisi ya kuongeza baadhi ya madini kwenye udongo ni kwakutumia majivu

UMUHIMU
Majivu yanakiwango cha wastani wa madini kifuatacho potasiam 5% - 7%, kalsiam 25% - 50%, fosforas 1.5% - 2% na madini mengine kwa kiasi kidogo pia mabaki mabaki ya chenga za mkaa kwenye majivu pia yanasaidia kwenye kunyonya baadhi ya sumu kwenye ardhi, kumbuka mkaa ni kaboni halisi (pure carbon)

KIASI CHA KUTUMIA
Kiasi cha kilo 2.5 mpaka 5 kitumike kwenye eneo la mita za mraba 33 au futi 100 za mraba, na majivu yamwagwe wiki 3 - 4 kabla ya kupanda kitu chochote ardhini.



MADHARA
Kila kitu kikitumiwa zaidi ya kiasi kina madhara na majivu pia yana madhara kwenye udongo kwa sababu yana hali ya kuwa alkaline zaidi (10 - 12 pH)  kwa sababu baadhi ya mchanganyiko wake hauyayuki kwenye maji, kama utahitaji kuongezea kwenye mimea yenye upungufu wa madini kama fosforas na potasiam basi hakikisha majivu hayagusi mashina kwani yanaweza kuuungua haya kama mimea ni michanga.

Pia majivu yanan kiasi kidogo sana cha naitrojeni ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya mmea wowote ule, kwa hiyo hakikisha pia unatumia vyanzo vingine kwa ajili ya naitrojeni, vyanzo kama mimea jamii ya mikunde, marejea,
 lukina , na alfalfa.

KILIMO BORA CHA MDALASINI-CINNAMON





Mti wa mita 10 au zaidi. Hutoa machipukizi na kuota miti zaidi ya mmoja kwenye shina moja na kuongeza mavuno mengi, haya mashina mapya yasing'olewe bali yaachwe yakue na kuwa mti mkubwa.


AINA
Mchanganyiko; za kienyeji (ndogo) na za kigeni ( kubwa)

HALI YA HEWA NA UDONGO
· Mvua nyingi za kutosha 2000mm -2500mm kwa mwaka
· Udongo wenye rutuba
· Joto kwa wingi
· Hewa yenye unyevunyevu

KUSIA MBEGU KWENYE VITALU
· Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa
· Sia mbegu kwenye kitalu zikiwa nusu sentimeta chini ya udongo
· Baada ya kuchipua, mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani
· Panda miche wakati wa masika
· Panda kwa nafasi ya 2m x2m. Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi. Nafasi kubwa hufanya miti kuwa na matawi mengi pia mashina hayanenepi wala kurefuka.





UTUNZAJI
· Acha machipukizi kwenye shina
· Toa matawi kwenye mashina ili kunenepesha mashina
· Weka shamba katika hali ya safi
· Zuia magonjwa kama.
- Vinundu (galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scales na mealbugs kwa kutumia dawa za sumu kama Selecron, Karate nk.

KUVUNA
· Anza kuvuna miaka 3 baada ya kupanda
· Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya miti
· Kata shina la mti,na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya
· Kuwa mwangalifu ili ganda litoke vizuri bila kupasukapasuka
· Seli za nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukaruza kwa kisu
· Kausha vizuri siyo kwenye jua kali Mavuno
· 0.25 kg – 10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja. Kiasi cha mazao hutegemea ukubwa na umri wa mti
· Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na umri wa mti. Mti wa umri mkubwa hutoa mganda yenye ubora wa chini.




MATUMIZI
Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa umesagwa au bila kusagwa hutumika kama:
· Kiungo kwenye chakula na vitafunwa kama keki, mandazi,vitumbua
· Vikolezo kwenye vinjwaji km. chai, kahawa
· Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya chakula
· Dawa ya ngozi

JINSI YA KUTUMIA
· kiungo kwenye chakula
Tumia maganda au saga magada yaliyokauka. Tumia ili kuongeza ladha kwenye vyakula kama pilau, ndizi, mchuzi nk 
· Kutengenezea kinywaji
Weka vipanda vichache 2-3 (30gm) vya maganda kwenye kikombe ongeza maji yanayochemka, funika kwa dakika 15, ongeza vipande vya limao. Kunywa kila baada ya kula.



MANUFAA
· Miti hudumu shambani zaidi ya miaka 20. Miti huchipua na kutoa machipukizi mengine kila baada ya kuvuna
· Gharama ndogo ya uzalishaji
· Mazao yaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu
· Magonjwa na wadudu ni kidogo
· Rahisi kuchanganya na mazao mengine
· Nguvu kidogo, kipato kikubwa.

ZIJUE FAIDA ZA KUTUMIA MATANGO KWA AFYA YAKO.




Watu wengi tunapenda matunda Fulani kwa ladha yake tuu bila kutaka kupata faida, katika mwili ikiwa faida ya baadhi ya matunda ni pamoja na  radha yamatunda  mabalimbali.

1.    Tango ni chanzo kizuri cha vitamin B.
2.    Tango huupa mwili na vitamin. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku.
3.    Tango pia hutumika kwenye matunzo ya ngozi/urembo ambapo huwekwa machoni na kuondoa vimbe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea kwani tango lina virutubisho vya kuondoa vimbe hizi na pia lina silicon na sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele.

4.    Tango lina virutubisho kama lariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol ambavyo kulingana na tafiti mbali mbali za magonjwa ya kansa husaidia kupunguza aina mbali mbali za kansa kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume.
5.    Tango husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani.
6.    Tango huondoa hangover kwa watumiaji wa pombe kwani lina vitamin B ambazo husaidia kupunguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka asubuhi ila unatakiwa kula kabla ya kulala ili uamke ukiwa vizuri.
7.    Tango husaidia kupungua uzito na mmeng’enyo uende vizuri. Kutokana na kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye tango na kiasi kikubwa cha maji, tango ni tunda sahihi kukusaidia upungue uzito. Kiasi cha maji kilichopo kwenye tango na Kamba Kamba zake huusaidia mwili kuondoa sumu katika mfumo wa chakula na kusaidia mmeng’enyo wa chakula. Unapokula tango kila siku pia hukusaidia wewe mwenye choo kigumu au usiyepata choo kabisa kwa muda mrefu kuondokana na tatizo hilo.



8.    Tango husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta mafuta kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote mbili (Low and high blood pressure). Tango lina hormone ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho (pancreatic cells) ilikuweza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari. Pia watafiti wamegundua kuwa kuna kirutubisho kiitwacho sterol kwenye tango ambacho husaidia kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu. Tango lina kiwango 
kikubwa cha potassium, magnesium na Kamba Kamba ambazo husaidia sana kudhibiti shinikizo la damu aina zote yani high blood pressure na low blood pressure.

Husaidia afya ya viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis). Tango ni chanzo kizuri cha silica ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo (connective tissue). Pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C & D, Folate, Calcium, Magnesium na potassium ambavyo hufanya tango linapochanganywa na juice ya karoti huweza kutibu gout na baridi ya yabisi (arthritis) kwa kupunguza kiwango cha tindikali kwenye mkoo (Uric acid).
9.    Kutokana na maji na virutubisho vilivyopo kwenye tango, tunda hili husaidia kupunguza homa pale inapopanda.
 Nadhani tutakuwa tumeelimika kwa kufahamu umhimu wa tunda aina ya tango ikiwa tunda hili halivutii kula kwa kuwa halina radha nzuri sana pia halina harufu inayosikia kuwa hili ni Tango  kwa kukazia tango lina asilimia kubwa ya maji.
Zingatia Madini ya Potassium yanayopatikana katika matango ndicho chakula cha moyo kwa sababu huwezesha moyo kupiga mapigo katika hali ya kawaida. Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha potassium kama tango ni muhimu sana hasa kwa mtu mwenye tatizo la moyo, shinikizo la chini la damu.

KILIMO CHA NYANYA TANZANIA




Utangulizi:

Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.

Uzalishaji wa nyanya duniani na hapa Tanzania

Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na Marekani, Italia na Mexico. Kwa upande wa Afrika nchi zinazo lima ni kama; Malawi, Zambia na Botswana. Zao hili hulimwa pia katika nchi za Afrika Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda na Tanzania.

Zao la nyanya linalimwa karibu maeneo yote ya Tanzania. Uzalishaji wa nyanya ni mkubwa kuliko mazao mengine ya mbogamboga yanayolimwa hapa Tanzania, uzalishaji wa nyanya kwa mwaka ni jumla ya tani 129,578 ikiwakilisha asalimia 51 ya mazao yote ya mboga. Kwa mujibu wa Wizara ya kilimo ya Tanzania maeneo yanalolima sana nyanya ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida. Morogoro ndiyo inayoongoza kwa kilimo hichi ikiwa na wazalishaji wenye zaidi ya hekta 6,159 (ekari 15,398). Pamoja na kwamba eneo la uzalishaji linaongezeka kwenye maeneo mengi lakini uzalishaji wa nyanya bado ni mdogo sana. 

Uzalishaji mdogo unasababishwa na kupungua kwa rutuba ya ardhi, upepo, joto, ukame. Sababu nyingine ni pamoja na ukosefu wa aina za nyanya zenye mavuno mengi amabazo zinahimili mazingira ya kwetu, wadudu, magonjwa na magugu.
Mazingira

Hali ya Hewa:

Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa n.k.)

Udongo:
Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 - 7.0.

Aina za Nyanya
Kutokana na tabia ya ukuaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawili:
1.    Aina ndefu ( intermediate) kwa mfano ANNA F1, Tebgeru 97. Aina hizi hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya greenhouse. Uvunaji wake ni wa muda mrefu, zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6, yaani hiyo miezi 6 ni ya uvunaji.
2.    Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx, Roma VF (nyanya mshumaa)
Kotokana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika makundi mawaili:
1.    1. OPV (Open Pollinated Variety) - Aina za kawaida
2.    2. Hybrid – Chotara: Hizi ni aina zenye mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu.
3.    Katika karne hii ya 21, nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa, zinazo zaa sana, na zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku nyingi bila kuharibika mapema.

Kuandaa Kitalu cha Nyanya
Mambo muhimu ya kuzingatia:
o    Kitalu kiwe karibu na maji ya kutosha na ya kudumu
o    Kiwe sehemu iliyowazi na yenye udongo ulio na rutuba ya kutosha
o    Eneo la kitalu kama ni kubwa liwe tambarare au na mwiinuko kidogo ili kuepuka maji yasituame kwenye kitalu, mtelemko ukiwa mkali sana nao sio mzuri kwani husababisha mmomonyoko wa udongo.
o    Kitalu kiwe sehemu ambayo haikuwa na zao la nyanya au viazi mviringo (au mazao ya jamii ya nyanya k.m. mnavu, biringanya n.k.)
o    Kiwe sehemu ambayo ni rahisi kupata huduma zote muhimu kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa miche kwenda sehemu nyingine. Pia kurahisisha usambazaji wa miche kwenda sehemu nyingine.

Kuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za Nyanya
Aina ya matuta:
– matuta ya makingo (sunken seed bed)
– matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed bed)
– matuta ya kawaida (flat seed beds)

Mambo Muhimu ya Kuzingatia wakati wa Kuandaa Matuta
Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ili mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni bila kukanyaga miche].o    Kwatua/lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini.
o    Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma 4-8 ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu.
o    Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/vunde au mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vizuri na udongo.
o    Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja (hatua moja) mraba.
o    Tuta lisiwe na mabonde mabonde au mawe mawe ambayo yanaweza kuzuia usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe vizuri ili kuhakikisha usambazaji mzuri wa mbegu na kuepuka mbegu kufukiwa chini mno kiasi ambacho hazitaota.

Faida na Hasara za Matuta yaliyotajwa hapo juu

1. Matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed beds);

Faida:
o    matuta ya namna hii huruhusu maji, hewa na mizizi kupenya kwenye udongo kwa urahisi zaidi.
o    mazao ya mizizi hupata nafasi ya kutosha kutanuka haraka zaidi
o    matuta haya hayatuamishi maji kama mengine, hivyo hutumika zaidi kwenye maeneo yanayokuwa na mvua mara kwa mara.
Hasara:
o    Matuta ya namna hii yana sababisha sana mmomonyoko wa udongo kama hayakutengenezwa vizuri.

2. Matuta ya makingo (sunken seed beds):

Faida:
o    matuta haya ni rahisi kutengeneza
o    hutumika wakati wa kiangazi ili kuhifadhi maji na unyevu
o    nyevu mdogo unaopatikana ardhini
o    ni rahisi kumwagilia kwa kutumia maji ya mfereji au bomba
o    huhifadhi unyevu nyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu
o    huzuia mmomonyoka wa ardhi
Hasara:
o    Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye
o    mvua nyingi.

3. Matuta ya kawaida (flat seed beds):
Faida:
o    ni rahisi sana kutengeneza kwani udongo ukisha kwatuliwa
o    na kusambazwa mbegu huoteshwa
o    ni rahisi kutumia eneo kubwa kuotesha mbegu

Hasara:
Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua nyingi.
Kusia Mbegu
o    Hakikisha ubora na uotaji wa mbegu kabla ya kuzipanda kitaluni (germination test)
o    Weka mistari kwenye tuta kulingana na ukubwa wa tuta, lakini mistari isiwe chini au zaidi ya sentimita 15-20 toka mstari hadi mstari
o    Kina cha mistari kisiwe cha kutisha bali kiwe kati ya sentimita 1-2
o    Matuta yapate maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu. Ni vizuri kutumia chombo cha kumwagilia (watering can).
o    Mbegu ziatikwe kwenye mistari na zisambazwe vizuri ili kufanikisha usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta. Changanya mchanga laini na mbegu kisha sambaza kwenye mistari iliyoandaliwa kwenye tuta.
Mbegu zinaweza pia kuatikwa kwenye tuta bila mistari, lakini zisambazwe kwa uwiano mzuri kwenye tuta ili kupunguza msongamano. Msongamano husabisha magonjwa ya fangasi kama vile kinyausi (damping off) au ukungu (blight).
o    Weka matandazo kiasi cha kutosha ambacho hakitazuia kuota kwa mbegu.
o    Mara baada ya kuatika mbegu, mwagilia maji kiasi cha kutosha kulingana na unyevu nyevu ulioko ardhini.



Mambo ya Kuzingatia baada ya kusia mbegu pamoja na Matunzo Kitaluni
o    Mwagilia maji kwenye kitalu baada ya kuotesha kulingana na unyevu nyevu uliopo kwenye udongo.
o    Miche yote ikisha ota, ondoa matandazo, kisha weka chanja ili kupunguza mionzi ya jua ambayo inaweza kuunguza miche michanga. (kipindi cha baridi si muhimu sana)
o    Punguzia miche (thinning) ili ibakie kwenye nafasi ya kutosha. Hivyo miche ibakie kwenye umbali wa sentimita 2.5 - 4. Hii itapunguza magonjwa ya ulemavu na mnyauko, pia itasaidia kupata miche bora na yenye nguvu.
o    Endelea kumwagilia hadi miche ifikie kimo kinachofaa kuhamishia shambani.
o    Punguza kiwango cha umwagiliaji maji, siku chache kabla ya kuhamishia miche shambani, yaani siku 7-10.

Kanuni na Mbinu za kuhamisha miche toka Kitaluni kwenda shambani (Transplanting
Rules)
o    Mwagilia miche masaa machache kabla ya kuhamishia miche shambani ili wakati wa kung’oa miche mizizi ishikamane vizuri na udongo.
o    Kabla ya kuhamisha miche, mashimo yawe yamekwisha andaliwa katika nafasi zinazo stahili huko shambani.
o    Miche ihamishwe wakati wa jioni ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na jua.
o    Kwa ujumla karibu mazao yote ya mboga mboga huwa tayari kuhamishiwa shambani yakiwa na majani kamili kati ya 2-6 pamoja na mizizi mingi iliyostawi vizuri.
o    Mche lazima uwe na afya nzuri, uwe umenyooka vizuri, hivyo miche yote iliyonyongea au myembamba kupita kiasi isichukuliwe wakati wa kupeleka shambani.
o    Ng’oa miche kwa uangalifu hasa pamoja na udongo wake kwa kutumia vifaa husika ili mizizi isidhurike.
o    Miche ihamishiwe shambani mapema mara baada ya kung’olewa toka kitaluni.
o    Wakati wa kuhamisha miche, uangalifu mkubwa utumike ili kutoharibu miche/mizizi.

Maandalizi ya Shamba la Nyanya


o    Shamba la nyanya liandaliwe mwezi 1-2 kabla ya kupanda miche.
o    Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya.
o    Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya.
o    Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60) x (50-75) kutegemeana na aina au hali ya hewa. Kama ni kipindi cha baridi ni vyema nyanya zikapandwa mbalimbali ili kuruhusu mzungungo wa hewa na kuzuia magonjwa ya fangasi.

Jinsi ya kupanda miche:
o    Hamisha miche toka kitaluni pamoja na udongo wake
o    Sambaza mizizi vizuri kwenye shimo bila kukunja.
o    Fukia miche kina kile kile ambacho shina lilikuwa limefukiwa bustanini.
o    Mwagilia maji ya kutosha kulingana na unyevunyevu uliopo kwenye udongo kasha weka matandazo na kivuli ili kupunguza uharibifu unaosababishwa na mionzi ya jua.

Mambo muhimu ya kuzingatia baada ya kuhamishia Miche Shambani
o    Kagua shamba mara kwa mara ili kujua maendeleo au matatizo yaliyoko shambani mapema
o    Hakikisha shamba ni safi wakati wote, palilia shamba na hakikisha magugu yote hasa yale ya jamii ya nyanya yamelimiwa chini.
o    Ondoa mimea iliyoshambuliwa na magonjwa au ondoa sehemu zilizoshambuliwa, kisha zifukiwe chini au kuunguza moto.
o    Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo na kusababisha mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya, hasa wale wanaopenda kiza na magonjwa yanayopendelea unyevunyevu.

Asante sana.