Watu wengi tunapenda matunda
Fulani kwa ladha yake tuu bila kutaka kupata faida, katika mwili ikiwa faida ya
baadhi ya matunda ni pamoja na radha yamatunda mabalimbali.
1.
Tango ni chanzo kizuri cha vitamin B.
2. Tango huupa mwili na vitamin. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku.
2. Tango huupa mwili na vitamin. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku.
3.
Tango pia hutumika kwenye matunzo ya ngozi/urembo ambapo huwekwa machoni na
kuondoa vimbe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea kwani tango lina
virutubisho vya kuondoa vimbe hizi na pia lina silicon na sulfur ambazo
husaidia ukuwaji wa nywele.
4. Tango lina virutubisho kama lariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol ambavyo kulingana na tafiti mbali mbali za magonjwa ya kansa husaidia kupunguza aina mbali mbali za kansa kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume.
5.
Tango husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani.
6.
Tango huondoa hangover kwa watumiaji wa pombe kwani lina vitamin B ambazo
husaidia kupunguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka asubuhi ila
unatakiwa kula kabla ya kulala ili uamke ukiwa vizuri.
7. Tango husaidia kupungua uzito na
mmeng’enyo uende vizuri. Kutokana na kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye
tango na kiasi kikubwa cha maji, tango ni tunda sahihi kukusaidia upungue
uzito. Kiasi cha maji kilichopo kwenye tango na Kamba Kamba zake huusaidia
mwili kuondoa sumu katika mfumo wa chakula na kusaidia mmeng’enyo wa chakula.
Unapokula tango kila siku pia hukusaidia wewe mwenye choo kigumu au usiyepata
choo kabisa kwa muda mrefu kuondokana na tatizo hilo.
8.
Tango husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta mafuta kwenye mishipa ya
damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote mbili (Low and high blood
pressure). Tango lina hormone ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho
(pancreatic cells) ilikuweza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti
kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari. Pia
watafiti wamegundua kuwa kuna kirutubisho kiitwacho sterol kwenye tango ambacho
husaidia kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu. Tango lina kiwango
kikubwa cha potassium,
magnesium na Kamba Kamba ambazo husaidia sana kudhibiti shinikizo la damu aina
zote yani high blood pressure na low blood pressure.
Husaidia afya ya
viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis). Tango ni chanzo
kizuri cha silica ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha
viunganishi vya viungo (connective tissue). Pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C
& D, Folate, Calcium, Magnesium na potassium ambavyo hufanya tango linapochanganywa
na juice ya karoti huweza kutibu gout na baridi ya yabisi (arthritis) kwa
kupunguza kiwango cha tindikali kwenye mkoo (Uric acid).
9.
Kutokana na maji na virutubisho vilivyopo kwenye tango, tunda hili husaidia
kupunguza homa pale inapopanda.
Nadhani tutakuwa
tumeelimika kwa kufahamu umhimu wa tunda aina ya tango ikiwa tunda hili
halivutii kula kwa kuwa halina radha nzuri sana pia halina harufu inayosikia
kuwa hili ni Tango kwa kukazia tango lina asilimia kubwa ya maji.
Zingatia Madini ya Potassium
yanayopatikana katika matango ndicho chakula cha moyo kwa sababu huwezesha moyo
kupiga mapigo katika hali ya kawaida. Ulaji wa matunda na vyakula vyenye
kiwango kikubwa cha potassium kama tango ni muhimu sana hasa kwa mtu mwenye
tatizo la moyo, shinikizo la chini la damu.
No comments:
Post a Comment